Ndoto za Kingi! Gavana wa Kilifi Amason Kingi adai hakuna corona kaunti hiyo

NA NICKSON TOSI

Gavana wa Kilifi Amasoon Jeffa Kingi sasa anasema kuwa hakuna kisa kingine kipya cha virusi vya Corona baada ya watu sita waliokuwa wamelazwa eneo hilo kutokana na virusi hivyo kutibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Wagonjwa hao walikuwa wamelazwa katika hospitali ya Jibana.

Kaunti ya Lamu ndio ya kipekee katika eneo la Pwani kutosajili ama kuwa na kisa chochote cha virusi vya Corona.

Yakijiri hayo, gavana wa Kwale Salim Mvurya ameitaka serikali kufunga kabisa mipaka inayoingia Kenya kwenye kaunti hiyo kutoka Tanzania. Mvurya amesema mpaka wa Lungalunga unawaingiza watu wengi eneo la pwani ambapo ni hatari kwa maisha ya kila mmoja nchini.