Nelson Havi achaguliwa rais wa LSK

Nelson Havi
Nelson Havi
Wakili Nelson Havi amechaguliwa rais wa chama cha mawakili nchini LSK .

Havi alishinda wadhifa huo katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali na kuwapiku wapinzani wake watatu. Amechukua wadhifa huo kutoka kwa Allen Gichuhi ambaye amehudumu kwa muhula mmoja. Mpinzani wake Havi Charles Kanjama na seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen ni miongoni mwa waliomhongera  kupitia twitter kwa ushindi wake .

https://twitter.com/ckanjama/status/1233071708627750913

Baada ya miezi minne ya kampeini kali Havi alifaulu kuwazidi Harriette Chiggai, Maria Mbeneka na Charles Kanjama.

Havi atahudumu kwa muhula wa miaka mitatu utakaoanza mwaka huu na kutamatika mwaka wa 2022. Chini ya sheria za sasa za LSK rais wa chama hicho huhudumu kwa muhula mmoja pekee. Takriban mawakili 10,764 wenye vibali vya kuhudumu walishiriki uchaguzi huo wa maafisa wao wapya .

https://twitter.com/kipmurkomen/status/1233078738344083458