NHIF kulipa gharama za wagonjwa wa Covid-19 KNH, Mbagathi

NHIF
NHIF
Hazina ya kitaifa ya matibabu NHIF  itagharamia huduma za matibabu ya  wagonjwa wa virusi vya coona katika hospitali za umma .

Kupitia taarifa kutoka kwa afisa mkuu mtendaji  Peter Kamunyo ,NHIF imesema  itawasaidia wote waliopatikana na virusi hivyo  na waliolipiwa  ada za kila mwezi ambao  watalazwa katika hospitali zilizoidhinishwa na wizara ya afya .

Hospitali hizo ni  ; Kenyatta National Teaching and Referral Hospital, Kenyatta University Teaching Referral  ,Research Hospital na Mbagathi County Hospital.

Nyingine ni hospitali za kaunti na taasisi nyingine za matibabu zenye idhini ya kuwahudumia wagonjwa wa Covid 19

"NHIF  haitagharamia bili zitokanazo na kulazwa katika hopitali ambazo hazijaidhinishwa na wizara ya Afya’ amesema Kamunyo .

,wezi machi kampuni za kutoa huduma za bima zilikubali kugharamia matibabu ya coronavirus baada ya  mashauriano .