Nia ya kuzima ndoto ya Ruto. TangaTanga waelezea hofu yao kuhusu ukimya wa Uhuru Kenyatta

Wandani na marafiki wa karibu wa naibu wa rais William Ruto sasa wanahoji kuwa kimya cha Rais Uhuru Kenyatta kimekuwa kingi mno.

Wanasema kwamba Uhuru sasa atoe taarifa kuhusu mahusiano yake na Ruto.

Baadhi yao ni wabunge katika mrengo wa Tangatanga ambao wanasema kwamba wanapata maonevu serikalini kwa sababu ya kufanya msimamo wa kumuunga mkono Ruto.

Soma hadithi nyingine:

Wanasiasa hawa sasa wanateta kuwa Uhuru asuluhishe "maonevu yanayoendelea" dhidi yao na vyombo vya usalama.

Wandani hawa wa Ruto sasa wanahofia kimya cha Rais Kenyatta ni ishara kwamba ametoa amri kwa wizara ya usalama wa ndani kuwanyanyasa wafuasi wa TangaTanga.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Nyandarua Faith Gitau amefunguka kwamba sio siri vikosi vya polisi na serikali nzima kwa kiujumla imezamia siasa za kumtafuta atakayemrithi Kenyatta.

Soma hadithi nyingine:

Gitau alimtaka rais kutangaza msimamo wake kati ya kumuunga mkono Ruto au kinara wa upinzani Raila Odinga.

Mbungwe wa Mukurwe-ini Anthony Kiai alidai kuwa kuna njama ya kulemaza juhudi za wandani wa Ruto.

“Rais anatakiwa atokee na kuongea na Ruto. Amewaacha wakenya kubashiri mwelekeo wa msimamo wake.

Lazima wakae pamoja na watuambie msimamo wao wa kweli."

Soma hadithi nyingine:

Mbunge wa Kandara Alice Wahome alitoa madai kwamba katibu wa kudumu Karanja Kibicho alifanya mkutano na wafanyabiashara tajika kutoka kaunti ya Murang’a wikendi iliyopita kupanga "njama ya kumzuia Ruto kumrithi Uhuru."

Mwanasheria huyu amesema kuwa mkutano huu uliendelea hadi saa saba usiku. Swala jingine lililozungumziwa pale ni pamoja na kuzima cheche za mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro .

Wawili hawa ni wandani wa Ruto.

Soma hadithi nyingine:

“Mkutano uliofanyika ulijadili jinsi ya kuzima ndoto ya Ruto kuwa rais. Aidha walijadili kuwa mimi na Ndindi Nyoro tunafaa tuzimwe kupitia lolote lile hata kwa kuuawa." alisema Alice Wahome