Mbusii Deh

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

Katika kikao cha Papa Na Mastaa wiki hii ilikuwa zamu ya mtangazaji Mbusii kufika na kujumuika katika shoo yake Rais Papa inayoruka kupitia mtandao wa Youtube wa Radio Jambo.

Papa hutumia fursa hii kuhoji mastaa kuhusu maisha yao ya muziki, mahusiano na mitindo. Mbusii ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Mbusii Na lion TekeTeke, alisimulia mwanzo mwisho kuhusu alivyoanzia utangazaji katika kituo cha utangazaji cha Ghetto.

Soma hapa mengine :

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

“Nilifanya miaka miwili kama office messenger na miaka tatu katika utangazaji.”

Mbusii alielezea Papa jinsi alivyokuwa muigizaji wa vitabu vya riwaya vya shule ya upili na baadaye kupata kazi katika Radio Jambo kituo kinachoendeshwa chini ya mwavuli wa kampuni ya Radio Africa Media Group.

Staa Mbusii ni miongoni mwa watangazaji hapa nchini ambao wamewekeza kwa kiwango kikubwa katika tasnia ya burudani kwa kuanzisha kampuni inayofahamika kama Hakuna Mbrrcha Entertainment. 

Katika kampuni hii, Mbusii ameweza kuajiri vijana wengi wakihudumu kama madeejay, wasanii wa kurekodi miziki kati ya maswala mengine tofauti.

Soma hapa:

Mercy Masika speaks about how song, ‘Mwema’ changed her life

Kuhusu mahusiano Mbusi alisema kuwa ingawaje ana mke na watoto hawezi kuwafungia nje mabinti warembo katika mahusiano.

“Watoto wa kike hiyo ni kiumombasani…nikiingia Mombasani nione Fatuma unadhani nitawabania kweli? Siwezi wabania lakini nikona bibi na watoto.”

Tazama mahojiano yetu naye.

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments