Nilianzisha 'Marini Naturals' baada ya baba kuugua saratani - Michelle Ntalami

Katika kitengo cha Ilikuaje hii leo mgeni wetu alikuwa Michelle Ntalami, mrembo ambaye ndiye muanzilishi na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mafuta ya asili ya nywele, Marini naturals.

Ntalami alifichua kuwa alianzisha kampuni hiyo takriban miaka minne iliyopita na alisema kuwa kilichompa msukumo ni wakati babake mzazi alipopatikana ana ugonjwa wa saratani (cancer).

"Babangu alikuwa ameugua saratani na nikaamua kutotumia kemikali kwani huharibu ngozi yangu. Nikaanza kuchanganya kemikali tofauti asili pamoja na mimea na hapo nikagundua kuwa naweza jiundia mafuta yangu ya ki asili.

Wazazi wake ndio waliompa fedha takriban millioni tatu na baada ya kuweka kama akiba alipata mkopo na hapo akaanzisha kampuni yenyewe.

Kulingana na Ntalami, marini ni jina la swahili linalomaanisha urembo wa ki asili.

Pamoja na wakurugenzi wenzake, wamefungua duka kadhaa humu nchini na wamefanikiwa kusambaza bidhaa zao katika nchi zaidi ya kumi barani Afrika.

Tuna duka moja The Junction, Ngong road pia tuko kwenye maduka kadhaa ya jumla nchini kote na pia katika nchi kumi na mbili kwa jumla.

Ntalami ambaye ana urembo wa malkia alifichua kuwa hana mchumba huku akidai kuwa alikuwa naye kabla yao kutengana miezi mitatu iliyopita.

Kwa vile macho ya umma yameniangazia, sipendi kuzungumzia mambo yangu ya uhusiano kwani mimi hupenda yawe siri.

Lakini sina mpenzi kwa sasa kwani nilitoka kwa mahusiano miezi mitatu iliyopita.

Kama mwanamke saa zingine mambo ya hisia hukulemea sana haswa, kikazi na biashara. Kwa mfano mimi ni mwanamke ambaye natilia bidii sana kwa kila kitu na saa zingine mapenzi hunyakua bidii ile.

&t=1049s