black man 2

‘Niliachwa na mke wangu baada ya kukatwa sehemu zangu za siri kwa ajili ya kansa.’ Jamaa asimulia jinsi upasuaji wa Penectomy

Victor Kabaka* yungali na maswali mengi kuhusu hatua ya mke wake wa miaka 10 kumuacha pindi tu alipogundua kwamba  madaktari walikuwa wameamua kumkata sehemu yake ya uume kwa sababu ya kansa.

 

‘Majambazi wa genge nilokuwa nikiongoza walimbaka dadangu,najutia usiku huo wa uhalifu’

Masaibu yake yalianza wakati alipoanza kuugua na kisha kupimwa na kupatikana na saratani ya sehemu yake ya uume. Iligunduliwa kwamba kansa ilikuwa imeathiri sehemu kubwa ya uume wake na  chaguo lilikuwa kuikata kabisa kupitia upasuaji kwa jina la kiingereza  Penectomy. Hakuamini  alipoarifiwa habari hizo na alipewa muda wa kuamua endapo angeidhinisha oparesheni hiyo au la kwa sababu endapo uume wake haungekatwa basi ingekuwa mwisho wa maisha yake. Baada ya majadiliano na familia yake na kubainika kwamba hapakauwa na njia nyingine iliamua kwamba oparesheni hiyo ingefanyika na akahamishwa kwenda  katika hospitali moja India  ambako upasuaji wa kuukata uume wake ulifanyika. Upasuaji wenyewe ulihusisha kuonodoa uvimbe uliokuwa  ndani ya misuli ya sehemu hiyo na hata mizizi inayoshikilia uume wake kwa mwili iling’olewa.

‘Mwajiri wangu alinitaka nifanye mapenzi na mbwa wake.’ Mkenya aliyekwenda Bahrain kufanya kazi asimulia masaibu yaliyompata

Bila kujua kitakachofuatia, mkewe Victor hakuwa amejitayarsha kuishi na mume asiyeweza kumpa tendo la ndoa na kwa bahati nzuri, Victor alikuwa na watoto wawili aliopata kabla ya kupata kansa.  Miezi miwili tangu aliporejea nchini na kuanza kupata nafuu, wengi walishangaa jinsi Victor na mkewe wangeendelea kuishi pamoja kama mke na mume hasa baada ya upasuaji huo.‘ Kilichofanya mke wangu kuniacha ni maswali ya mara kwa mara kutoka kwa watu wakiwemo majirani  waliotaka kujua iwapo kuna njia ya mimi naye kuendelea kushiriki tendo la ndoa,’ anasema Victor.

Unaogopa kusema ‘I love you?’ Hizi hapa namna za kumuonyesha mtu unampenda bila kutamka lolote

Anasema alifikiri baada ya miaka 10 ya ndoa walikuwa wamejenga  uhusiano thabiti  ambao haungetikiswa na oparesheni aliofanyiwa kumbe hakujua umuhimu wa tendo la ndoa kwa mkewe. Kuondoka kwa mkewe ghafla kumemuacha Victor katika hali ya kutojifahamu kwani haamini kwamba licha ya  kutatizika kiakili kwa ajili ya kukatwa uume wake, sasa pia atasalia bila mke na katika hali yake itakuwa vigumu kumpata mwanamke atakayeishi naye kutokana na hali yake. Je, ungejipata katika hali ya Victor ungefanya nini?

 

 

 

 

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments