''Nilikuwa nakataliwa!'' Aliyekuwa mwigizaji wa Real Househelps of kawangware afunguka

Esther Chebet ajulikanaye kama Matilda katika kipindi cha Real Househelps of Kawangware  ni binti mwenye kipaji si haba.

Kidosho huyu alifanya kazi kama mwigizaji katika kipindi cha RHK kwa muda wa miaka mitatu kabla ya kuacha kuagiza mwaka wa 2017.

https://www.instagram.com/p/By2eE_iAbsF/

Baada ya kuacha, binti huyu alianza kuigiza katika kipindi cha Sue na Johnie kinacho peperushwa kwenye stesheni ya Maisha Magic kisha baadaye akaacha.

Baada ya kuacha uigizaji, binti huyu alijitosa kwenye lindi la vichekesho na mpaka wa sasa yeye hutengeneza video mbalimbali za kuchekesha na kuziweka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
Akizungumzia safari yake ya uigizaji, binti huyu alisema kuwa, alikuwa anafanya kazi kwenye 'Cyber' na kuwa hakuna siku amepata matatizo kuzungumza na watu kwenye mitandao.
''I USED TO WORK IN A CYBERCAFE AND HAVE ALWAYS BEEN AN ONLINE PERSON. I FIND IT EASY INTERACTING ONLINE.''

Chebet ambaye alianza kuigiza akiwa na umri mchanga alisema kuwa, mwalimu wake ndiye aliyeona talanta ile kwake mwaka wa 2019 alipokuwa kidato cha tatu.

Vilevile, alisema kuwa alienda kwenye ukaguzi mara nyingi lakini hakufaulu ata siku moja.

''I WENT FOR SEVERAL AUDITIONS BUT WAS REJECTED EVERY TIME I TRIED. THERE NO AUDITION I’VE ‘WON’ EITHER FOR FEATURE, DRAMA OR FILM.''Esther alisema.

Licha ya hayo, alizidi kusema kuwa, katika sanaa hii ya uigizaji, hufai kuwa mtu mnyonge sana kwani mambo hayatakuwa rahisi kwako na kwake yeye, kuilichomfanya afike alikofika ni uraibu wake wa kujipa moyo.

''I FEEL THAT I HAVEN’T EXHAUSTED MY POTENTIAL FOR THE TWO ROLES I’VE PLAYED [IN REAL HOUSEHELPS AND SUE NA JOHNIE]. I HAVE SO MUCH POTENTIAL AND NEED TO GET MORE ROLES. I ALWAYS FEEL I NEED TO GO FOR MORE AUDITIONS SO AS TO GET ROLES.''

Zaidi ya hayo,binti huyu alisema kuwa amepitia mengi kutoka kwa mashabiki wake. Wengi wamemtia aibu kupitia mitandao ya kijamii lakini hajakufa moyo.

''I’VE BEEN BULLIED, BODY SHAMED. MOST OF THEM USE PSEUDO ACCOUNTS. I RESPOND TO TROLLS’ COMMENTS AND BLOCK AFTERWARD. SOME OF THEM I JUST IGNORE.''

Aidha, Esther alisema kuwa vichekesho vyake vingi huwa kwenye lugha ya kikalee.