massawejapanni (1)

‘Nilimwagia mpango wa kando wa bwanangu acid,’ Afunguka Mercy

Wanajambo, haswa kinadada wamekuwa wakifunguka kuhusu vitendo walivyo tekeleza ili kupambana na wapenzi au ukipenda mipango wa kando wa wapenzi wao.

Hapo jana mwanadada kwa jina Joyce aliwashtua wengi alipokiri kuwa pindi tu alipojua mumewe ana mpango wa kando, alikata kauli na kumtafuta na kumvamia licha ya kuwa yule mwanadada alikuwa mja mzito.

Patanisho: Ni upuzi tu! Mume afunguka kuhusu kuwa na mpango wa…

Leo tunaangazia mwanadada kwa jina Mercy ambaye alifanya mabaya zaidi ikilinganishwa na bi Joyce.

Anasema kuwa yeye alimfumania mpenziwe na mpango wa kando na badala ya kupambana na jamaa, aliamua kumvamia maskini mwanamke yule.

Mercy anasema alipigiwa simu na kuarifiwa kuwa mpenziwe wa miaka miwili yuko mahali na mwanadada fulani, hapo akafunga safari na kununua asidi. Baada ya kumpata aliamua kumwagilia usoni na kutimua mbio kwani anakiri hakuwahi tiwa nguvuni.

Licha ya hayo yote wawili hao walitengana na kwa bahati mbaya, yule jamaa akafa maji na kumuacha Mercy na mtoto wao mmoja.

Mwanaume mwenye swag! Ommy Dimpoz aonyesha ustadi wake

Soma usimulizi wake Mercy,

Unajua niliitwa nikaambiwa ako mahali fulani, nikaenda nikabuy acid na nikamwagia usoni. Sikushikwa kwani nilimwagia nami nikajipea shughuli lazima kila mtu apambane na hali yake.

Tulikuwa tumeishi naye kwa mda wa miaka miwili, alikuja akafa maji sasa sahii nina mtoto wake.

Papa Francis kuruhusu wanaume waliooa kuwa mapadri

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments