Nilinyang'anywa mke na Shamba boy - Reuben

sad
sad
Je waweza hisi vipi mke wako akinyakuliwa na jamaa mwingine? Isitoshe akinyakuliwa na mfanyikazi wako?

Basi jamaa kwa jina Reuben aliwacha mtangazaji, Massawe Japanni na huzuni baada ya kusimulia jinsi mkewe alitekwa na shamba boy au ukipenda mfanyikazi wa nyumbani.

Kulingana na Reuben, mkewe alikuwa na tabia ya muvizia vizia mfanyikazi huyo kila anapo ondoka na kuelekea kazini. Siku moja aliporejea nyumbani aliwafumania wakiwa kitandani huku wakiwa wamewekeleana miguu.

Anasema licha yao kushtuka, bado waliendeleza uhusiano wao kisiri na siku moja mkewe akaondoka na yule shamba boy.

Kisa hicho kilitendeka miaka miwili iliyopita na Rueben anadai alibahatika kubaki na wanao wawili. Hata hivyo anasema kidonda kila hakijapona bado na hana nia ya kutafuta mke mwingine.

Soma usimulizi wake,

Mimi nilikuwa naishi na mke wangu na nikaleta mfanyikazi kijana kwa boma ili afuge ng'ombe, ashughulikie mahindi na pia kufanya usafi.

Lakini mwenye nalaumu sana ni mke wangu, kumbe wakati nilipotoka alikuwa anajaribu kufinya macho kwa ule kijana, imagine wakaanza uhusiano. Mimi nikienda napata iko hivi, imagine niliwapata kitandani wamewekeleana miguu na walishtuka sana.

Iliendelea ivo na nikajaribu kuwaonya ikashindikana, imagine iliendelea ivo na ikafika mahali, kusema ukweli huyo kijana alienda na bibi yangu na nimebaki mwenyewe.

Nilipokonywa bibi na shamba boy. Nikipigia mke wangu simu ni kama ameniweka blacklist na sasa nimeamua kuishi hivyo na mungu mwenyewe atajua.

Tulikuwa na watoto wawili na nilibaki nao nikiwashughulikia wakiwa shule. Nakwambia hawa watu wanaleta shida.

Tangu anifanyie hivi miaka miwili imeisha, na sahii sijapata mwingine nimeamua kuishi hivi na kukaa kama kijana wa boma.