Nimehamasishwa na maisha yake Bob Collymore, Nameless asema

65394445_461981021260942_8924921809264155508_n
65394445_461981021260942_8924921809264155508_n
Ibada ya kukumbua maisha ya Bob Collymore ilifanyika jana katika Kanisa la All Saints Cathedral. Familia na marafiki walihudhuria na kumpa heshima zao mwisho.

Viongozi wa biashara maarufu na wanasiasa pia walikuwa miongoni mwa washiriki. Wasanii pia hawakuachwa nyuma. Miongoni mwa wale waliohudhuria walikuwa Juliani, Nameless na mke wake Wahu.

Nameless aliandika na kusema,

"Leo ninapoketi hapa katika ibada hii nahamasishwa na aina ya maisha uliyoishi kwani uliyaadhiri kwa njia njema maisha ya wengi ikiwemo kaka yangu na utu wako mzuri. Tunakusherehekea. Pumzika kwa Amani,"
Juliani, ambaye alikuwa rafiki wa karibu na mkurugenzi mkuu wa Safaricom, alisema kwamba wakati analia, anakumbuka kwamba hilo ndilo jambo la mwisho angetaka.
Aliendelea na kusema,
"Asante sana kwa kufungua mikono yako, nyumba yako, maisha yako, na mawazo kwangu mimi. Ulipenda kila mmoja wetu kwa makusudi ,mke wako Wambo na watoto, wafanyakazi wenzako na nchi yako Kenya."