"Nimemuua. Sasa kujeni mniue," Mshukiwa awapigia simu polisi

Madai ya chanzo cha kifo cha mama na binti yake  yamechukua mkondo mpya baada ya ripoti za uchunguzi kuonyesha kwamba huenda mama alinyongwa na mwanawe kabla ya kujitoa kitanzi.

Judith Wanjiku ambaye ni mfanyakazi wa zamani wa hazina ya kitaifa pamoja na binti wake Catherine Nyaguthie walipatikana katika nyumba yao mtaa wa Golden Gate South B wakiwa wameaga dunia.

Wachunguzi  wanasema kwamba simu ya marehemu ilitumiwa kuwapigia polisi kwa nambari 112 mnamo Septemba 21.

Soma hadithi nyingine:

Aidha, polisi wanashuku kwamba aliyewapigia simu ni binti yake marehemu.

Ufichuzi huu umewafanya wachunguzi wa  mauaji hayo  kufutilia mbali tetesi kwamba waliuliwa na waliokuwa katika   gari aina ya Toyota Prado.

Awali ilikisiwa  kwamba  wanawake hao waliouliwa na watu hao waliowasafirisha hadi mtaa wao usiku wa manane, siku chache tu kabla ya mili yao kupatikana.

"Nimeua. Sasa kujeni muniue" hayo ni maneno yaliyodhaniwa ni mzaha wakati polisi walipopigiwa simu.

Soma hadithi nyingine:

Ufichuzi zaidi unaonesha kwamba Judith Wanjiku mwenye umri wa miaka 73 huenda aliuliwa na binti yake katika  nyumbani kwao Nairobi.

Marehemu alikuwa akikaa  na  binti yake pamoja na  muwewe aliyekuwa amelazwa hospitalini wakati huo.

Polisi wanasema kwamba  walipigiwa simu na mtu aliyedai kuwa ametekeleza mauaji hayo Jumatatu asubuhi.

Ripoti za kina kutoka polisi zinaonyesha kwamba Catherine Nyaguthii mwenye umri wa miaka 47 huenda alimwuua mama yake mzazi kabla ya kujitoa uhai.

Soma hadithi nyingine:

Mauaji hayo yanadaiwa kuchochewa na sababu ambazo hazikufahamika mara moja.

Inakisiwa kwamba  Nyaguthii alijiua kwa kunywa sumu kwa kuwa hakuwa na alama yoyote  au ishara ya kutokwa na damu mwilini.

Polisi walipigiwa simu saa chache kabla ya mili yao  kupatikana kila moja ndani ya chumba chake katika nyumba yao yenye majumba manne.

Miili hiyo ilitambuliwa na jamaa wao mnamo Jumatatu.

Maongezi katika ya polisi na mshukiwa yalirekodiwa kwa simu na kutumwa kwa maafisa wa  DCI kwa uchunguzi zaidi.

Kuibuka kwa ushahidi huu upya unafutulia mbali tetesi kwamba wanawake hao waliuliwa na watu waliokuwa katika gari aina ya Toyota Prado.

Soma hadithi nyingine:

Wachunguzi walichukua kanda za video za CCTV ili kubaini mmliki pamoja na watu walikouwa katika gari hilo.

Zaidi ya hayo, watu wengi wamehojiwa  na polisi kuhusuiana na maafa hayo, miongoni wao ni walinda lango wa mtaa huo, majirani pamoja na jamaa wa marehemu.

Mwili wa Nyaguthi ulipatikana sakafuni huku ukiwa umelala kifudifudi.

Nao  mwili wa mama yake ulipatikana katika chumba cha kulala, huku kamba ikiwa imefungwa shingoni mwake, Pia kitanda chake kilikuwa kimeloa damu.