Nimepata Watoto Na Makabila Ya Luo Na Kikuyu Na Sina Shida Yeyote! Annita Raey Akemea Ukabila

Mtangazaji wa kipindi cha Sema Na Raey, ni miongoni mwa watu wachache mashuhuri ambao wamejitokeza kukandamiza machafuko machache yaliyoripotiwa ya baada ya uchaguzi uliopita wa ki rais, nchini.

Maeneo kadhaa humu nchi yaliadhirika sana huku wananchi wa jamii tofauti wakizozana matokeo yakiwa uharibifu wa mali, chuki na pia vifo.

Annita Raey ambaye amekuwa katika mstari wa kwanza kushurutisha wakenya kutofwata uchochezi wa wanasiasa wanaohubiri chuki na machafuko, aliamua kuzungumzia swala hilo huku akiwaomba wazazi kutowatumbukiza wanao kwenye janga la kikabila.

"Huu ugomvi kati ya Luo na Kikuyu sijui ulitoka wapi na wengi wetu tulizaliwa tukaupata lakini tumeharibu mambo zaidi." Alisema Annita.

Sisi wenyewe tumeoa au kuolewa kutoka hizi jamii au wengine wetu tumejaliwa watoto kutoka jamii tofauti. Kwa mfano mimi ni mkikuyu na watu wengi hawana habari. Nina mtoto wa kiume ambaye babake ni mkikuyu na mtoto wa kike ambaye babake ni Mluo.

Msichana wangu hajui babake ni mluo na mamake ni mkikuyu na sasa kwa wenye wanasema kuwa hawataki wajaluo au wakikuyu waniambie, mtoto wangu nitamgawanya aje mara mbili nusu moja ielekee Karachuonyo huku nusu nyingine ielekee Kiambu? Twafaa tuwache ukabila!

Aliongeza Bi. Annita akisisitiza kuwa jina halifai kuwa shida katika nchi hii kwana sisi wote ni ndugu na dada.

Tazama kanda ifuatayo.