“Nina mtoto wangu alipata Corona, mtoto wa kuzaa mimi.''- Asema Magufuli

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amefichua kuwa mwanawe ambaye alikuwa ameambukizwa virusi hivyo sasa amepona na yupo hai.

Amesema mwanawe ambaye hakumtaja jina alijitenga ama kujifungia kwa nyumba akitumia dawa za kiasili pamoja na maji ya limau kujitibu .

“Nina mtoto wangu alipata Corona, mtoto wa kuzaa mimi, amejifungia kwenye chumba akaanza kujitibu, akanywa malimau na tangawizi, amepona yuko mzima sasa anapiga push up,” alisema Magufuli alipokuwa akihudhuria misa kanisani.

Magufuli ambaye ameshutumiwa kwa siku za hivi karibuni kutokana na utepetevu wake kuhusiana na virusi hivyo hatari, amesema anapania kufungua shule na hata michezo kuendelea katika taifa hilo.

Akiendelea kusema kuwa corona ni kama magonjwa mengine, hatakubali virusi hivyo ambavyo vimeathiri mataifa mengi ulimwenguni kuathiri uchumi wa taifa lake.

“Hatuwezi kubali Corona itawale, Mungu wetu atatawala… Tumekuwa na magonjwa kama ukimwi…,”  amesema Magufuli.

Hivi maajuzi alitupilia mbali vifaa vilivyokuwa vinatumika kuwapima watu Tanzania akisema havikuafikia viwango vya kutosha .

“There is something happening. I said before we should not accept that every aid is meant to be good for this nation,” Magufuli alisema akiongezea kuwa vifaa hivyo vilivyotumika kuwapima wagonjwa wa virusi hivyo ni sharti vichunguzwe.