"Ninazo jumbe za sauti na kanda zinazoonyesha njama ya kuua Ruto,"- Dennis

ruto_william_tears
ruto_william_tears

Dennis Itumbi sasa anasema kuwa ana uwezo wa kuonyesha jumbe za sauti na kanda zinazoonyesha waziwazi mpango mzima wa kumuaa naibu wa rais William Samoei Ruto. Dennis aliomba apewe nafasi kuzicheza jumbe zile katika mahakama mbele ya jaji akisema kuwa wapelelezi walifahamu kuwa anazimiliki.

“Ninazo sauti na kanda kwa mujibu wa upelelezi zinazoonyesha kuwa mkutano ulifanyika hoteli ya La Mada na ndani kuna mazungumzo yanayoonyesha uwezekano wa kumwangamiza naibu wa rais."Alisema Dennis.

Soma hapa:

Mwanastratejia huyu wa maswala ya kidijitali alitiwa nguvuni katikati mwa jiji la Nairobi jumatano ili kuhojiwa kuhusu barua ghushi inayoonyesha njama na mpango wa kumuua William Ruto.

Dennis alifikishwa kortini Alhamisi na kuagizwa akae ndani korokoroni kwa siku 14 katika kituo cha polisi cha Kamukunji akisubiri upelelezi kutamatishwa.

Hakimu Zainab Abdul aliagiza mwanablogu huyu kufungwa kifungo cha siku 5 katika kituo cha polisi cha Muthaiga.

Soma hapa pia:

“Siku 14 ni nyingi zaidi kwa kuwa upelelezi ulianza Juni 20. Simu ya mshukiwa pia imechukuliwa kwa uchunguzi zaidi." Zainab Abdul.

Inakisiwa kuwa Itumbi aliandika barua hiyo na ndani kuifanya ionekane chanzo chake ni mawaziri waliandika.Kuna madai kuwa Itumbi alikosa kushirikiana na makachero huku akikataa kurekodi kauli na maafisa wa polisi. Dennis alikana madai haya.

Kiongozi wa upelelezi Yvonne Anyango alisema kuwa madai yanayomlenga Itumbi yana uzito mkubwa na ni tishio kubwa kwa usalama wa taifa na yanaweza kuchochea vurugu nchini.

 Kesi hii inatarajiwa kutajwa Julai 10.