Nishawahi kuwa ‘MBOCH’:Zari Hassan atoa ufichuzi kuhusu maisha yake ya hapo awali.

zari 1
zari 1
Mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan  kwa mara ya kwanza ametoa ufichuzi kuhusu jinsi alivyopitia maisha magumu hapo awali kabla ya umaarufu na   amafanio ambayo ameyapata kupitia shughuli zake nyingi .Kupitia ujumbe katika Instragram Zari  ,mama ya watoto watano amesimulia jinsi alivyowahi kufanya kazi ya nyumba nchini Uingereza  ili kujikimu kimaisha .

https://www.instagram.com/p/B7GgKX2HMDI/

Zari ameelezea kujitolea kwake kufanya kazi za hapa na pale huku akiendelea  na masomo yake ili kuboresha maisha yake na familia yao hasa baada ya babake mzazi kuondoka na mamake akifanya kazi kama mshonaji .

‘Nilisikitika sana kumwona mamangu akiteseka kila uchao’ amesema Zari katika ujumbe huo mrefu ambao pia umevutia hisia mbali mbali za mashabiki wake ambao wamesifia ujasiri wake . Akiwa Uingereza ,Zari amesema alikuwa akiishi na shangazi yake ambaye alimchukulia kama mtoto wa kambo ,hali inayoonyesha huenda alipitia mateso . Lakini ukakamavu wake na bidii vimemfikisha alipo sasa na ujumbe wake amesema unalenga kuwapa watu zaidi ari ya kutaka kufaulu maishani .