" Nitahakikisha hauna nafasi yoyote Kenya," Ruto amfokea Raila

unnamed__1561985990_75568
unnamed__1561985990_75568
Naibu wa Rais William Samoei Ruto ammepiga kijembe kiongozi wa upinzani Raila Amollo Odinga leo kwa kumwambia kuwa lengo lake ni kuwafanya wakenya wawe maskini ili wamtegemee.

Soma hapa:

Ruto alionekana kumjibu Raila baada Odinga kusema jumamosi kuwa viongozi wanaotoa kitita kikubwa cha pesa katika harambee za kanisa nchini wanapaswa watangaze asili ya utajiri wao. Ruto alisema haya akiwa katika hafla ya kukuza pato la kina mama Mugirango kaskazini, kaunti ya Nyamira.

"Ulikuwa unapinga Eurobond ukisingizia ufisadi; ukapinga pia Northern Collector Tunnel bado ukisema kuna ufisadi; Ulikuwa unapinga reli ukisingizia ufisadi; bado ulikuwa unapinga kutoa pesa kanisani ukisema ni ufisadi." alifoka Ruto.

Soma hapa:

"Ni kwa sababu wewe ni "mungu wa umaskini" na unataka ukata katika nchi hii. Unapinga kila mradi wa maendeleo nchi hii ili watu wawe maskini ili wazidi kukufuata na mimi nakwambia tutafanya kazi usiku na mchana tuuondoe umaskini. Hautakuwa na nafasi yoyote nchi hii." Ruto alimwambia Raila.

Ruto mara kwa mara ametetea kitendo chake cha kutoa hela kusaidia miradi kanisani na kusema hawezi goma kufanya hivyo.