Njambi Koikai, mwanamke aliyepitia upasuaji mara 21

Njambi Koikai amekuwa akiugua ugonjwa wa endometriosis kutoka wakati alipokuwa kijana.

Katika safari yake, amekuwa akizungumza na kuelimisha umma kutumia kurasa za vyombo vya habari vya kijamii, hasa Instagram.

Kwenye ukurasa huo, anasimulia umma anachopitia.

Alitoa wito mbele ya gavana wa Mombasa Allan Hassan Joho  ambaye alichanga shilingi milioni 1 baadaye.

Sasa Njambi anataka kuonekana kwenye kipindi cha Marekani cha Ellen Degeneres show.

Njambi alimtuma ujumbe wa kihisia kwa Ellen kwa matumaini kwamba angeweza kuonyeshwa katika kipindi chake, ambacho kina umaarufu zaidi.

Aliwauliza wafuasi wa Instagram kumsaidia kufikisha neno kwa Ellen.

Hapo awali alimtumia Ellen barua.

Barua yake ilisoma 

Dear Ellen, my name is Njambi Koikai from Nairobi Kenya, a stage four thoracic endometriosis survivor. Endometriosis is a disorder in which the tissue that normally lines the uterus grows outside the uterus. In my case the endometriosis spread all the way to my lungs, diaphragm, chest, ribs, appendix and close to my heart.
(Ellen mpendwa, jina langu ni Njambi Koikai kutoka Nairobi Kenya, niko katika hatua ya nne ya ugonjwa wa endometriosis. Endometriosis ni ugonjwa ambao tishu za kawaida ambazo huukuza tumbo ya uzazi hukua nje. Katika kesi yangu endometriosis ilienea sana kwa  mapafu, kifua na karibu mwa roho yangu.)
Njambi aliendelea kusema amepigana na ugonjwa huo wa endometriosis kwa miongo miwili na amefanyiwa upasuaji 21 hadi sasa.
Wakenya waliyoiona video yake walimhimiza Ellen kumpa nafasi kwa kipindi chake.