Nusura nijitie kitanzi,Asema Maureen Waititu

maureen
maureen
NA NICKSON TOSI

Mwanablogu na mtangazaji wa Televisheni  Maureen Waititu ameelezea kisa chake ambapo alijaribu kujitia kitanzi mara mbili .

Akizungumza wakati wa mahojiano na televisheni moja ya humu nchini,mama huyo wa watoto wawili alisema kama hungekuwa uwepo wake mwenyezi ,sasa hivi hangekuwa yuko hai.

Alielezea kuwa wakati mmoja aliamua kuendesha gari lake kwenda kujitoa uhai lakini kukaanza kunyesha na kuamua kurejea nyumbani ambapo aliketi maeneo ya kugesha gari kwa kina na kuanza kulia .

“Grace I’ll be honest, I almost took my life twice and each time it was like God was like what you think you are doing. There is a day he intervened I was just gonna drive off somewhere and it started raining and it poured and poured and I just drove back. Sat and cried in eyes out in the parking lot and it did not stop raining. It was on a Sunday I won’t forget. At that point you know after letting it all out, there is some calmness that comes over you and I was like where am I even going? I went back to the house and I found my son waiting for me,” Alisema Waititu.

Katika mahojiano hayo ,Waititu alielezea jinsi babake mzazi alivyomkataa wakati alipoukuwa mchanga na hata alipokua mtu mzima swala ambalo liliathiri mahusiano yake na mpenziwe Frankie Justgymit.