Nyakati za mwisho za E-Sir, Nameless afichua jini la E-Sir la mfuata

Mwimbaji mashuhuri Nameless ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuonana na mwanamziki aliyetazamiwa sana E-Sir, kabla ya kifo chake cha ghafla.

Ni zaidi ya muongo moja tangu mwanamziki huyu ambaye alikuwa anapata umashuhuri kwa kasi sana kupoteza maisha yake kupitia ajali ya barabara mwezi wa Machi 16, 2003.

Alikuwa njiani akirudi Nairobi kutoka kwa tamasha Afraha Stadium, mji wa Nakuru ambapo alikuwa anasaidia ku uza albamu ambayo nyimbo zake zimebaki kuvuma kwenye vilabu leo.

E-Sir alikuwa motisha na mshauri si kwa watu wengi pekee ila pia alikuwa ni taswira ya wasanii wachanga waliokuwa wanachipuka na miziki ya kisasa.

Alikuwa amefanya kazi pamoja na Nameless kama vile Boomba Train ambayo itabaki milele kwenye historia.

Nameless anamkumbukia pacha wake katika mziki ambaye walikuwa wanatawala naye siku hizo.

''Nilipatana na E-Sir Splash (Langata) baada yake kujiunga na Ogopa na tukawa marafiki. Tungefanya maonyesho pamoja na baada ya hapo tungekaa chini na kujadili jinsi onyesho lilikuwa.

''Tungesafiri kwa matwana na abiria wengine wangeskia nyimbo zetu na kuzikejeli bila kujua kuwa tumeabiri nao. Angeskia watu wakisema jinsi wanachukia mtindo wa mziki wetu kwa kuwa tulikuwa tunaufanya tofauti na E-Sir angeniambia baadae, 'hawa watu wana chuki sana, tuungane na tuwe jina kubwa'.''

Hivo ndivyo nyimbo zilizotamba kama Boomba Train na Maisha zilizaliwa. Boomba ilifanya vyema sana kwetu, hadi sasa imekuwa ngao yangu na hunipa nguvu kuendelea na tamasha zangu kwa sababu inaongelea vitu ambavyo tulikuwa tukiongelea, mapambano na jinsi tulitaka kuziepuka.

'' Nilipoanza matembezi ya ziara na E-Sir nilikuwa jina tajika kwenye kiwanda cha mziki hivyo nilihakikisha kuwa nimefunga tamasha ili kudumu mashabiki wetu. Angeanza nami ningemaliza kisha ningemuita tuigize Boomba Train.''

Nameless aliongeza, ''tulikuwa Nakuru, tamasha yetu ya mwisho  na E-Sir. E-Sir alikuwa akisoma kiwanda hiki cha mziki haraka na kurekebisha uandishi wake. Nakumbuka baada ya tamasha kadhaa alikuwa amekuwa jina kubwa na sasa yeye ndiye alikuwa akifunga. Siku hiyo alitamatisha tamasha kisha nikaja baadae kufanya Boomba Train,'' Nameless akumbukia.

Nameless aliandika chini kuhusu mkasa huo wa ajali ambao ulichukua maisha ya E-Sir.

''Sikujua kutoka wakati nilipelekwa hospitali yote yaliyotendeka. Niliambiwa alikuwa hospitali tofauti na sikuwa na simu ama jinsi ya kuwasiliana naye.''

Aliendelea, ''Ndugu yangu alikuja kutoka Nairobi. Nilimuliza kila mtu lakini hakuna aliye niambia. Ndugu yangu ndiye aliniambia, 'E-Sir hakufanikiwa'. Haikuizama ndani yangu. Unajua vizuri ulikuwa na mtu kisha unaambiwa kuwa hayuko tena, haikuzama ndani.''

Akiongeza, ''nilibadilisha na nikaingia kwenye gari na hapo ndipo Boomba Train ilichezwa, na kile ninacho kumbuka ni watangazaji wakiitangaza. Katika muda huo nilivunjika moyo na hapo ikazama. Nililia na nilipokua nikiuskiza mzika wake ukicheza ningehisi kuwa alikuwa anaongea na mimi.''

Nameless alisema kuwa maisha baada ya E-Sir kuaga haijakuwa rahisi.

''Kusonga mbele bila yeye ilikuwa ngumu kwa muda. Mke wangu huwa ananiambia kuwa kitu ndani yangu ilibadilika. Ilinichukua nyuma na nakumbuka nikienda kufanya wimbo kwa makumbusho yake.

Alimalizia, ''nakumbuka nikifanya tamasha, bado nilikuwa na jeraha, lakini nilipofika kwenye jukwa upendo niliokuwa nao kwa E-Sir ulinifanya niseme ingawa ameenda lazima ningeendeleza wosia wake.