Odi wa Murang'a ashtumiwa kwa utapeli na B Classic

Msanii B Classic alimshtumu msanii wa bendi ya Boondock,Odi Wa Murang'a kwa kumtapeli,B Classic alisema kuwa Odi alilipwa shillingi 25,000 kufanya kazi naye.

B Classic aliposti 'screenshot' za pesa alizotumiwa kwa njia ya Mpesa mnamo Juni,14,2020, huku zikielezea maelewano kuwa Odi alikuwa arekodi mistari katika collabo hiyo ya wimbo huo.

Makubaliano yao yalikuwa kuwa Odi aandike baadhi ya mistari ya muziki huo, na kisha ajitokeze kwenye video ya kibao hicho lakini alienda kinyume cha makubaliano yao na kurekodi mistari ya wimbo huo na wanamuziki wengine.

Odi alirekodi kibao kinachofahamika kama Dubbed bleki, akiimba mistari aliolipwa na studio ya Champions.

Hii hapa audio ya kibao hicho;

&feature=emb_title

"Tunamtaka Odi aweze kuto kibao hicho kwenye mitandao ya kijamii au alipe studio ya Champions kwa uharibifu alioufanya." B Classic Alizungumza.

Odi hakuweza kupokea simu zetu wala kujibu jumbe zetu ili atoe maoni kuhusu madai hayo.

Hiki hapa kibao ambacho alitoa kinyume na Studio ya Champions;

&feature=emb_title