Ojaamong atishia kuwaondoa mamlakani wabunge wanaokosoa kazi yake

Mbunge wa Matayos Geoffrey Odanga amekosoa vikali matamshi ya Gavana Ojaamong kutishia kuhakikisha kuwa wabunge wanaokosoa utendakazi wake kutoka kaunti ya Busia wanaondolewa malakani ifikapo mwaka 2022.

Odanga amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kwa gavana Ojaamong kudai mbele ya wenyeji wa Busia, kuwa hatua ya baadhi ya wabunge kutoka kaunti hiyo kukosoa utepetevu unaoshuhudiwa kwenye serikali yake ni kinyume cha seria haswa swala la serikali hiyo kukosa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka miwili, licha ya miradi hiyo kutengewa fedha.

Akizungumza mjini Busia, mbunge huyo amesema kuwa ni jukumu lao kama wabunge waliochaguliwa na wananchi kufichua uovu wowote katika serikali ya kaunti, huku akimtaka gavana Ojaamong kutilia maanani malalamishi ya waakilishi wa wadi katika bunge la kaunti ya Busia.