Olunga kapewa ofa ya kubadilisha uraia wake? Gidi na Ghost wasimulia

Siku kadhaa zilizopita, kulikuwa na tetesi nyingi kuwa mshambulizi matata wa Harambee Stars, Michael Olunga alipewa ofa ya euro 600, ambayo ni kitita cha bilioni 67.7, ili abadilishe uraia wake.

Tetesi hizo ambazo zilibainiwa kutokuwa na ukweli wowote, zilienezwa na tovuti ya updates.co.ke, zikisema kuwa Olunga alipewa ofa hiyo ili abadilishe uraia na kuwa wa Japan.

Habari hizo zilijia baada tu ya Olunga mwenye miaka 25, kufunga mabao manane pale timu yake Kashiwa Reysol ilipowanyuka Kyoto Sanga mabao 13-1.

Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi, watangazaji hao waliangazia swala hilo na Gidi alipoulizwa kama angebadilisha uraia wake alipeana masharti ambayo yanaweza mfanya afikirie kuhusu ofa hiyo.

"Kwanza kabisa kama wanaweza badilisha chakula chao, siwezi ishi nchi ambayo wanakula nyoka." Alisema Gidi.

Aliongeza,

Wakiweza kuweka ugali na kuku ile ya kienyeji, na mrenda na osuga halafu na pilipili kwa umbali, naweza kuwa japanese."

Skiza kanda ifuatayo.