Orodha ya wote waliofariki katika ajali iliyomuua Kobe Bryant (PICHA)

kobe bryant
kobe bryant
Nyota wa mpira wa vipaku nchini Marekani Kobe Bryant na binti yake Gianna ni miongoni mwa watu tisa waliofariki katika ajali ya helikopta iliyotokea mji wa Calabasas, California.

Bryant amefariki akiwa na miaka 41, alikuwa anasafiri na ndege binafsi aina ya helikopta ambayo ilianguka na kuwaka moto. Mkuu wa polisi wa LA anasema kuwa hakuna yeyote aliyenusurika ajali hiyo.

Ripoti za awali zilisema kuwa kulikuwa na watu watano ndani ya ndege. Bryant, ambaye ni bingwa wa NBA mara tano alikuwa anatambuliwa duniani katika historia ya kuwa mmoja wa wachezaji bora wa vikapu.

Ifuatayo ni orodha watu wote walio aga katika ajali hiyo.

Kobe Bryant

Gianna Bryant

John Altobelli- babake Alyssa

Keri Altobelli- Mamake Alyssa

Alyssa Altobelli- mchezaji mwenza wa Gianna Bryant

Christina Mauser- kocha

Sarah Chester- Mamake Payton

Payton Chester- mchezaji mwenza wa Gianna Bryant

Ara Zobayan- rubani