Oscar Sudi adai ingekuwa makosa Ruto kuhudhuria kongamano la Covid-19

Ni kongamano ambalo lilikuwa limesubiriwa sana na wananchi huku naibu wa rais William Rut akisusia kuhudhuria kongamano hilo huku wandani wake wakimuunga mkono na kusema hakukua na haja yake ya kuhudhuria kongamano hilo kwa maana alikuwa tayari ametengwa na serikali yake.

Mbunge wa Kapseret, Oscar Sudi amesema angelimvua Naibu wa Rais William Ruto taji la kuongoza vuguvugu la "hustler" endapo angelihudhuria kongamano la kitaifa la COVID-19.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter Sudi alidai kuwa ingekuwa kosa kubwa kama Ruto angehudhuria kongamano hilo.

"Endapo William Ruto angefanya makosa kuhudhuria Kongamano la COVID, ningempokonya taji la hustler na kuwania urais. Hatutaki upumbavu." Aliandika Sudi.

https://twitter.com/HonOscarSudi/status/1310685249706352644

Kabla ya hafla hiyo kuanza, Makamu wa Rais alikuwa ametengewa kiti chake na alikuwa amejumuishwa kwenye ratiba na kupewa jukumu la kumkaribisha kiongozi wa taifa kutoa hotuba yake.

Jukumu la Ruto lilikabithiwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i ambaye alimkaribisha Rais.

"Sasa wanataka kujifanya Ruto alikosa hii? Baada ya kumtenga kwenye mikutano yao tangu Machi wakitaka kutumia janga hili kung'aa sasa ufanisi wao ni wizi KEMSA. Unataka kutumia Ruto kutakaza uovu? Hapana." KImani Ichungwa Aliandika kwenye mtandao wake wa twitter.