Otile Brown hatimaye amezindua albamu yake

Album-Cover-Otile-Brown
Album-Cover-Otile-Brown
Hatimaye albamu ya Just In love iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wakenya kutoka kwa msanii Otile Brown imezinduliwa.

Albamu hiyo ya nyimbo 10 ni ya kwanza kwa msanii huyo tangu kutia guu katika sanaa ya muziki nchini mwaka 2015. Katika muda huo Otile amejiweka katika ramani nzuri ya ya wanamuziki wanaofanya vyema nchini.

Kwenye albamu hiyo Otile amewashirikisha wasanii kama vile Mejja, Khaligraph, Juma Jux ,Meddy kutoka Rwanda na msanii Kidum.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa albamu hiyo alikuwa na haya ya kusema;

“My fans should be prepared for a musical feast for the senses. Expect nothing but flames! I believe from this album, I’ll be able to win over new fans, because the vibes are different from what many are used to.”  Amesema Otile.

Ameongezea kuwa nyimbo zilizoko kwenye albamu hiyo zinaangazia maswala ya kuhusiana na mapenzi.

“Just In Love” explores themes of love and the relationship between men and women, while drawing inspiration from a variety of different musical genres, from R&B to Afropop.  Amesema Otile.

Miongoni mwa nyimbo ambazo zipo katika albamu hiyo ni kama  “Regina”, “Hit and Run”, “Leila”, “Dusuma”, “Pretty Gal” and reggae infused “Umedamshi”, “Dede”, “Kosea”, “Watoto Na Pombe” na  “Zaidi Yako”.

Otile amesema kutokana na marufuku ya kutangamana katika maeneo mbalimbali ya mikutano, mitandao yake ya kijamii itamfaidi pakubwa kuhakikisha kuwa wanaomfuatilia wamepata kufahamu kila kitu atakachokuwa anapania kukifanya.