Otile Brown na Sanaipei ni wapenzi? Ujumbe wa Otile waibua hisia

NA NICKSON TOSI

Nabayet kichuna kutokea Ethiopia anaendelea kumtumia Otile Brown jumbe za mapenzi lakini huenda jumbe hizo hazitasitisha dhamira na lengo la msanii Otile la kuanza kutafuta mahaba kwengineko baada ya wawili hao kuwa katika patashika za hapa na pale kwa muda.

Jumapili Otile alipofahamu kuwa yeye na msanii Sanaipei Tande walizaliwa siku moja, alimuandikia ujumbe ulioibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki wao na pia wakenya walioanza kufikiria kuwa huenda Otile alikuwa ameanza kuonyesha nia ya kummezea mate kichuna huyo walioshirikiana naye kutoa wimbo wa Chaguo la Moyo.

Otile alianza kwa kujiandikia ujumbe wa kusherehekea kwa siku yake ya kuzaliwa kisha Sanaipei akafuatisha ujumbe wake, mazungumzo yaliyoibua hisia miongoni mwa watu.

Mungu nashukuru kwa siku hii spesheli maishani mwangu licha ya kuwepo na mkurupuko wa Corona 🙏.aliandika Otile

Sanaipei-Ewe! Kumbe siku moja kabla ya yangu?!! 😂 Happy birthday!

Otile-@sanaipeitande labda 😊

Sanaipei-🤣🤣 ushaanza!! Enjoy!

Baada ya gumzo hilo,Otile aliamua kumuandikia Sanaipei ujumbe wa kumtakia siku njema ya kuzaliwa ujumbe ulioonekana kama wa kibinafsi baina ya wasanii hao wawili.

Huu hapa ujumbe huo.

"Heshima yako totoz , Dah!sikufahamu kuwa tunasherehekea siku ya kuzaliwa siku moja, labda ndio maana tunatoa nyimbo nzuri na ushirikiano wetu wa kuimba huwa wakupigiwa mfano... utasalia kuwa rafiki wa karibu wa kike kwangu... Happiest birthday. Nakutakia siha njema, baraka tele katika shughuli zako na maisha mema, nakupenda ❤️," aliandika Otile

Wengi waliona ujumbe huo na walikuwa na haya ya kusema .

itongwa_mb Chaguo la moyo ❤️❤️

robbie_king96 Ufisi detected 😂😂😂🇰🇪🇰🇪🇰🇪

richdolittle Otile …Pete  ikam thru joh😂😂😂👏👏👏😋🤗

Mhariri; Davis Ojiambo