Paka Mwitu Ashambulia Na kuumiza Watu Wawili Rongo

paka mwitu
paka mwitu
Watu wawili wanauguza majeraha katika hospitali ya gatuzi dogo la Rongo baada ya kushambuliwa na paka wa mwituni wakiwa njiani.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, paka huyo aliwashambulia wawili hao David Ododa na Joyce Atieno Otieno baada ya kutokea kwenye shamba la miwa lililokuwa karibu na barabara hiyo ambayo walikuwa wakipitia.

Mmoja wao Joyce Atieno Otieno alishambuliwa na paka huyo ambaye alikwama kwenye mguu wake na alipopiga mayowe David Ododa pia alishambuliwa na paka huyo alipokuwa akijaribu kumnusuru Bi Joyce kutoka kwa mnyama huyo.

Wawili hao wanaendelea kupata matibabu huku polisi wakitaka shirika la huduma la wanyama pori KWS kumkamata paka huyo ambaye alitorokea kwenye shamba moja la miwa.