PATANISHO:Mume wangu aliniacha wacha nisaidiwe na wanaume alisema niko nao.

Katika kipindi maarufu nchini cha patanisho hii leo Kelvin,25, alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe,21, aliyekosana naye mwaka jana Octoba.

"Nilikosana na mke wangu, mwaka jana kwa sababu nilikuwa namshuku kuwa alikuwa na mipango ya kando, nilimsaidia mtoto wake akiwa mdogo sana kama wiki tatu

"Alienda kwao tulipokosana, kuna wakati alipigiwa simu na mwanaume akaniambia niseme kuwa mimi ni mjomba wake." Alisema Kelvin.

Lakini kilele kilifika pale mke wake alipigiwa simu na kukana madai hayo.

"Mimi sikuwa na wanaume bali ni yeye alikuwa ana leta wanawake kwa nyumba na kulala na wao, na pia nikiwa kitandani naye alikuwa anawatumia ujumbe wanawake nikimuuliza ananiambia kuwa ni rafiki yake mwanaume." Alieleza mkewe Kelvin.

Mkewe Kelvin alimaliza mazungumzo na kusema kuwa hataki kurudiana na Kelvin kamwe

"Wacha wanaume ambao anasema niko nao wanisaidie sitaki kurudiana naye kamwe hata asiwahi nipigia simu, kwa sababu hakunisaidia na chochote.

Mtoto wangu alikuwa na miezi tatu tulipooana, na hata hajawahi mnunulia nguo mtoto wangu alikuwa ananyonya kwa hivo hakula chakula chake." Alisema.

Aliongeza na kusema kuwa mume wake alikuwa ananunua chakula na hata kuenda kununua mboga hakuwa anampa fursa mkewe kufanya bajeti.