PATANISHO: Nilikuwa na lala kitanda moja na mke mwenza wangu

Katika kipindi cha  patanisho Wanja alituma ujumbe ili apatanishwe na mume wake David,29 waliokosana kutokana na mipango ya kando.

"Tulikosana na mume wangu miezi mitatu iliopita na mimi nikarudi nikaenda kwetu, alikuwa anakuja na wanawake kwa nyumba na tunatumia kitanda moja." Wanja Alieleza.

Wanja alizidi kueleza na kusema,

"Nilipoenda kwetu hata hajawahi nitumia ujumbe wowote wala kunipigia simu, na tumebarikiwa na watoto wawili." Alisema.

Alidai kuwa kuna msichana aliyefahamika kama Shiro alikuwa anampigia simu.

Mumewe alipopigiwa simu alisema,

"Wewe mwenyewe ndio ulijiondoa ukitaka kurudi rudi mwenyewe siwezi kujia, na huyo msichana anaitwa Shiro nilimwambia  kumhusu

Nilimwambia nitamletea mke mwenza na akakubali, na nilipomletea nilikuwa nalala kitanda moja na wao na kisha wakakosana baada ya siku tatu

Hata hakuwa na heshima ya wazazi wangu, alikuwa anawaongelesha vibaya, na sitamuendea ajirudishe kwa sababu sikumfukuza." Alieleza David.

Si hayo tu David alisema,

" Shiro ashaarudi kwao na nampenda kama vile nampenda Wanja kwa sababu wote wana watoto wangu." David Alisema.

Wanja hakusita na alikuwa na haya ya kunena.

"Kujirudisha itakuwa ngumu, mimi nataka anikujie niliku bali kuletewa mke mwenza kwa sababu amekuwa akinichapa kwa muda sasa." Alisema.

Wanja alishikilia kiki kuwa ni sharti mumwe afunge nyayo na kuelekea kwao ndiposa arejea kwa ndoa yao la sivyo atamshtaki kwa polisi na kuwachiwa jukumu la kuwalea watoto.

Upande wake  David alikata kauli na kusema hatamuendea mkewe Wanja bali ajirudishe jisnsi alivyojipeleka kwa sababu si mara ya kwanza kuenda kwao.