PATANISHO: nampenda sana mume wangu ilhali hunichapa

Mary,35, alituma ujumbe apatanishwe na mume wakebaada ya kukosana na mume wake Patty,44, na kumpeleka katika kituo cha polisi hapo jana kutokana na kichapo alichokuwa amempa.

"Jana nilipeleka mume wangu polisi kwa maana alikuwa ananipiga tangu mwaka wa ,2014, tumekuwa kwa ndoa kwa muda wa miaka saba

Niliamua tuachane lakini niksema si uamuzi mwem kwa sababu tumetoana mbali na amenitendea mambo mengi

Akikuja nyumbani kazi yake ni kuongea tu na wanawake, na pia ana mipango ya kando, alinioa na watoto." Alieleza Mary.

Mary alisema kuwa alimtumia ujumbe mumewe na kumwambia ataavya mimba yenyewe.

"Uwa anakuja nyumbani ananipiga akiwa amelewa, alafu anatoka anaenda kama wiki mbili, baadaye uwa ananiomba msamaha." Alisema.

Baada ya kujieleza mume wake alipigiwa simu bali ilikuwa imezimwa, Mary alikiri kuwa anampenda sana mumewe .

"Licha ya kunipiga na mimba ya kwanza kutoka, na mpenda sana na nilikuwa nataka kumuomba msamaha na  tufutilie kesi yetu mbali." Mary Aliongea.