PATANISHO: Angeline Amsamehe Fred Licha Yake Kumshuku Kuwa Na Mpango Wa Kando

Siku ya Jumatatu, Fred alijiunga na orodha ya wanaume walio na bahati sana nchini baaada ya mkewe, Angeline kukubali kumskiza na kumsamehe licha yake  kumshuku kuwa na uhusiano au mpango wa kando.

Fred ambaye ni mfanyibiashara anaye safiri masafa marefu mara kwa mara, alipashwa habari na rafikiye kuwa kuna mme mmoja ambaye alionekana kwake na baada ya kufanya utafiti wake akafikia kikomo kwamba mkewe alikuwa na mpango wa kando, kinyume na ukweli.

Kulingana na Angeline, dadake ndiye aliyekuwa na urafiki na jamaa mmoja na ni kisa hicho ambacho labda kilizua uvumi huo. Licha ya hayo, alimsamehe mumewe na kuahidi kurudi nyumbani ili wasuluhishe yote pamoja.

Pata uhondo kwa kanda ifuatayo.