pata.fresh

PATANISHO: Bibi yangu alihama na watoto

George alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Hellen, ambaye walitengana na kwenda na watoto na kwenda Nairobi.

“Ilikuwa mwezi wa nane mimi nafanya kazi Siaya na bibi anafanya Nairobi. Sasa nilikuwa nimeenda likizo pamoja na watoto Nairobi, sasa siku nilikuwa nirudi nyumbani nilipata kijikaratasi kilikuwa kimeandikwa mke wangu alikuwa ameenda Uganda.” Alieleza George.

Sasa kumuuliza alikataa kujieleza na nikamwambia kama amekataa kuniambia ukweli, ukirudi nyumbani tutaongea. Sasa wakati wa kuja alipeana watoto kwa ndugu yake na aliporudi akachukua watoto na baadaye ndio akaniambia ndoa yetu imeishia hapo.

Sasa on Sunday, nikasafiri Nairobi ili tuongee na nikapata tayari ameshahama. Nikaspend the whole day kumtafuta na sikumpata kwani sijui alikohamia. Jana nilimpigia simu lakini bado hajaniambia aliko.” Aliongeza jamaa mwenye umri wa miaka 30.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya mika saba na wamejaliwa watoto wawili.

Alipopigiwa simu bi Hellen alikiri amehama lakini atarudi tu kwani hamna tatizo haliwezi tatuliwa.

“Mimi nilikuwa nimemwambia kama anaweza ji sort na aendelee na maisha yake, nilikuwa tu nafeel nikae kivyangu. Gidi unajua kuna maneno mengine huwezi sema kwa redio, hadi nilimueleza mambo ya Uganda sio yalifanya tuachane.” Alisema Lenny.

Pata uhondo kamili.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments