PATANISHO: Bibi Yangu Alininyima Tendo La Ndoa Akidai Amerogwa

Bwana Dennis aliomba apatanishwe na mkewe akidai kuwa anapitia magumu baada ya mkewe kuondoka.

"Tulipata tatizo wakati alipata kazi ya house keeping. Nilipomtafutia hiyo kazi alibadilika pap! Sasa shida ikawa time zake za kurudi nyumbani hazikuwa zinajulikana, mara anarudi saa kumi na mbili, saa moja au hata saa nne." Alijieleza.

Lakini hilo halikuwa tatizo kuu kwani ni hali ya kutafuta riziki. Shida kuu ikawa sasa ni maisha yetu ya bedroom ilikuwa shida kabisa maana alibadilika na hayo maneno hataki. Ile jioni umemtreat vizuri kabisa, nampa vizuri nzuri build up inakuwa nzuri lakini ukifika pale inakuwa tatizo. Mimi kumuuliza anasema anashuku amerogwa. Aliongeza akidai kuwa walipigana sana na mamake aliskia.

Alisema kuwa ilifika mahali mkewe alichukua mali na kudai kutoweka kwao na hapo jamaa aliamua kujitenga na kuhama huku akibeba meza ya pasi na mkoba wa mavazi.

Wawili hao walikosana mwaka wa 2016 na hadi wa leo hajui kwenye mkeo yuko na isitoshe mkewe hataki maneno ya kurudiana.

Dennis na mkewe wamejaliwa na mtoto mmoja baada ya kuwa pamoja kwa miaka saba.

Alipopigiwa simu mama Domingo alisema hawezi rudiana na mumewe akidai kuwa Dennis huzungumza maneno machafu na kuwa ana tabia ya ugomvi.

"Hata kama unajaribu ku apologize kwa mtu si eti uanze kutumia insults. Mimi naweza tu kuwa rafiki naye lakini mambo ya mapenzi la." Alijieleza.

Pata uhondo kamili.

&t=306s