pata.pata

PATANISHO: Bwanangu alinifukuza na mtoto wangu usiku

Bwana David alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Teresia ambaye walikosania swala la marafiki ambao alikuwa anatembea nao.

“Aki nimekuja Radio Jambo kwa sababu tulizungumza na sielewi mbona hutaki kurudi. Aki nisamehe sitarudia tena.” Alijitetea David huku Teresia akimshawishi atafute mke mwingine kwani amechosha na vituko vyake.

“Sasa wewe unajua makosa yako na wacha nikwambie, wewe tafuta bibi mwingine wachana na mimi. Mimi nimesha move on kwa sababu mimi siwezi ishi na wewe. Hakuna mambo ya kushinda nikirudia vitu wewe unajua kenye nilifanya kwa hivyo nimechoka, wachana na mimi.” Alisema Teresia kabla ya kukata mawasiliano.

Kulingana na David yeye hana habari ni nini haswa alifanya na anataka aambiwe ili ajirekebishe kwani alifikiri ni kitu kidogo kiliwakosanisha.

Nilikuwa nachelewa nje na marafiki zangu, saa zingine nakosa kazi mchana na inapatikana jioni na sikujua mambo yalikuwa yamefika hapo.” Alijitetea bwana David.

Teresia alisisitiza kuwa bwanake alimuoa na mtoto na hamtaki kwani akipata shida hataki kumsaidia.

Nikimwambia mtoto ana shida hataki kuskia kwani ana biashara ya pikipiki lakini hataki kumsaidia hata fare ya mia mbilihawezi nisaidia. Isitoshe kuna siku alinifukuza na mtoto usiku.” Aliongeza Teresia.

Pata uhondo kamili.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments