PATANISHO: Bwanangu ana tabia ya kubugia pombe na kunipiga

Charleson alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe ambaye walitengana kwa ajili ya tabia zake za kubugia pombe.

"Mke wangu nimemuoa kwa mwaka mmoja. Nafanya kazi za dereva wa masafa marefu na nikirudi nyumbani naeza pata mke wangu hayuko na huwa ni mzozo mtupu." Alieleza Charleson.

Naweza mpata hayuko kwa nyumba na unaweza pata ameenda salon au kwa marafiki zake na sasa huwezi jua kama ni ukweli. Juzi nilirudi kwa nyumba nikapata hajapika, kumuuliza akaja juu na nikakasirika nikampiga na akaondoka.

Nimejaribu kuzungumza naye lakini hata akiona simu yangu anakata, sometimes ananiambia atarudi atarudi lakini leo ndio nataka aniambie kama atarudi ili nijue la kufanya.

Charleson ana miaka 25, na mke wangu ana miaka 22. Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitatu na wana mtoto mmoja.

Alipopigiwa simu bi Faith alisema mumewe huwa na tabia za kulewa na kumpiga. Isitoshe huwa hamjali.

Faith alimueleza kuwa atarudi nyumbani.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be