PATANISHO: Bwanangu anapenda moshene na mipango ya kando

gidi patanisho
gidi patanisho
DOH! Nimejaribu kujenga boma langu lakini bwanagu anabomoa. Hayo ni madai mama Brayo alidai katika kipindi cha patanisho hii leo.

Bwana Patrick kila mchana anaonekana na wamama, akitembea nao wakipiga moshene na isitoshe one week baada ya kuolewa alipatikana na mpango wa kando.

Wololo! Hivi ndivyo Bwana Patrick alimwelezea Gidi.

'Tulikosana nikamchapa, na baadaye nikadhani amenisamehe. Aliambiwa na majirani wetu eti nilikuwa na mpango wa kando na nilionekana nikinunua condom. Alidai kuwa nilikuwa na mpango wa kando na nilipatikana nikinunua condom kwa duka, tukabishana nikimwambia awache kuskiza wengine'.

'Kwa bahati mbaya nikampiga na umbrella, Bibi yangu amehama na mtoto wetu, na vitu vyetu pia, na sijui mahala ako.Hata wazazi wake hawajui pahali alipo, anaficha alipo. Mke wangu anaskiza maneneo ya watu wa nje, kwa mfano aliambiwa na mwenye duka kwamba nilionekana nikinunua condom. Ilileta shida na mke wangu kuhama, nimejaribu kuongea naye lakini hasikii'.

Mama Brayo amemshika mara kadha na mipango ya kando, one week baada ya kuolewa nilimshika na mpango wa kando wakinyonyana barabarani.

'Niliwachana na huyo kwasababu nilitaka kuwa nioleke. Mara ya pili nikampata na mpango mwingine. Mara ya tatu niligundua mapngo wake baada ya mwenye duka kuniambia kwamba bwanangu hununua condom kwa duka yake. Hiyo kitu iliniuma nikamuuliza bwanangu. Baadala ya kunijibu, aliamka akanipiga na chuma, nikaumia kwa mabega.

'Alinitandika mara ya pili, na hakuna mahali nilienda. Bwanangu ameshinda akiniambia nitoke nyumbani kwetu, na siku moja nilibebea vitu zangu na mtoto pia'.

Bwana Patrick aliomba msamaha kwa mama Brayo, akisema binadamu hukosea. 'ile kitu nataka ni tukae kwa amani na tulee mtoto wetu. Tusahau yaliyo'.

Skiza kanda ifuatayo;