PATANISHO: Bwanangu hanitetei licha ya mateso ya wakwe zangu

Kennedy alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe wa miaka kumi bi Faith ambaye walikosana wiki jana.

"Mke wangu ameenda nyumbani bila any valid reason. Nafanya kazi Eldoret na serikali ambapo tumeishi naye miaka kumi na nikahamia Kisumu ili nijijenge, naye nikaamua akae nyumbani." Alieleza Ken.

Kuna dadangu ambaye ana mtoto kule ambaye amewachia mama mzazi, kuna wakati mamangu akienda mikutano humuachia mke wangu mtoto wa dadangu na lile halikumfurahisha.

Sasa nikaenda kule na nikamkanya mamangu na hapo ikasemekana kuwa tunamsengenya na mke wangu na ikaleta maneno." Aliongeza akidai kuwa mke wake alibeba watoto na kwenda kwao.

Juhudi za Ken kumtafuta mkewe hazijafua dafu kwani hata amejaribu kujipanga kusafiri kwao lakini mkewe anamkanya.

Alipopigiwa simu bi Faith alisema kuwa hataki kuzungumza na mumewe kwani atanena uwongo tupu na kuwa mumewe ana ukora chungu nzima.

"Mimi nilimwambia tuwache mambo ya wazazi tuwache na tuishi maisha yetu." Alisema Faith huku akisisitiza kuwa ni kama mumewe aliogopa kumpeleka nyumbani kwao kwa ajili ya kabila lake.

Alisisitiza kuwa mama na dada mkwe wamempa mateso pale nyumbani na mumewe hafanyi juhudi za kumtetea wala kumpa maisha bora.