PATANISHO: Charles Amsamehe Eliza Na Kumchukua Kama Mke Wa Pili

Kama ilivyo ada, patanisho la jana halikukosa vituko vya kila aina, na haswa siku hiyo ikiwa siku kuu ya ndugu zetu waislamu, sikukuu ilitamba kwote kwa wasikilizaji wa Radio Jambo na pia kwa wapenzi wawili, Eliza na bwanake Charles.

Eliza 22, alituma ombi la kupatanishwa na Charles 28, ambaye walikuwa wamekosana na kutengana kwa takriban mwaka mmoja.

Kulingana na mwanadada huyu, bwanake Charles ambaye walikuwa wameoana tangia mwaka wa 2011 alimpiga na kumkata kwa upanga baada ya "Babake Charles kusingizia kuwa nilionekana na kijana mwingine." Na baada ya hayo yote bwanake alioa mwanamke mwingine na isitoshe Eliza yuko tayari kurudiana naye na kuwa mke wa pili.

Baada ya kumpigia Charles simu, alikariri kuwa mkewe ndiye aliyekuwa na tabia ya mipango ya kando na mda mmoja aliolewa na rafikiye Charles kabla ya kurudi kwao. "Baada ya hayo nlimchapa kofi na ndipo alipo angukia upanga kwa bahati mbaya na ukamkata wala sikuchukua upanga na kumkata." Alisema Charles.

Huku akiendelea kukariri, Charles alisema licha ya matukio hayo yote, Eliza aliendeleza tabia hizo na hapo ndipo wawili hao walipotengana.

Baada ya ushawishi mkuu kutoka kwa watangazaji Gidi na Ghost, Charles hakuwa na budi ila kumsamehe Eliza na kumkubali kama mke wa pili.

Pata uhondo kamili katika kanda ifuatayo.