Patanisho: Evans alimfumania mke wake kitandani mwao na jamaa flani (AUDIO)

Gidi alishikwa na butwaa aliposome ujumbe wa bwana Evans na vile alipopata mke wake akishirika ngono na jamaa flani pale mtaani.

Akieleza kilichotokea, Evans alisimulia kwamba alimfumania mke wake Josephine Evans ni mwanajeshi na kuna wakati alipewa off na mke wake hakutarajiwa Evans atakuwa off. Hapo ndipo alimpata mkewe na mtu fulani wakiwa katika hiyo hali.

Evans wa miaka 26, alibishana na huyo jamaa, na mwishowe bibi yake pia akatoka na huyo jamaa.

Wawili hawa wana mtoto mmoja, na baada ya kuka miezi kadha bila bibi, Evans akaamua heri mke wake arudi nyumbani.

Kisa hiki kilifanyika mwaka 2015, na hawajaonana.

Je anadhani mkewe atarudi?

'Hiyo ndio sijui sababu nikimpigia simu  saa zingine anashika nikumuuliza penye ako, saa zingine ni Mombasa, so nikumuuliza nikuje huko tuongee, ananiambia wacha nitakuaambia'. Sometimes anaweza kukosa kuchukuwa hiyo simu, iko hivo.'

Na mkewe amekuwa akifuatilia kujua hali ya mtoto?

'Labda ananipigianga, ama anaendaga huko nyumbani kuangalia mtoto, hivo hivo tuu.'

Na yule jamaa ambaye alimfumania pale kwake hasikii maneno yake. Hajui kama ameoleka au sio.

Je Evans alimshawishi mke wake arudi nyumbani? Skiza kanda ifuatayo, ujuwe kilichotendeka.