PATANISHO: Gidi kama uko upande wa Nancy nitakata simu!

Ikiwa siku ya Jumanne, aliyeomba kupatanishwa hii leo ni bwana Anthony akisema alikosana na mkewe bi Nancy Nekesa, mwezi wa saba mwaka huu.

"Makosa ni eti mimi nilikuwa mahali kwa kikao nakula vitu vya wazee na kulikuwa na mrembo fulani. Sasa nilikuwa na motorbike na mimi humbeba kama mteja wangu."Alisema Anthony.

Licha ya kumwambia ukweli akasema tutengane na nilimwambia tutaumiza watoto wetu, nimekuwa nikimfuatilia nikimbebembeleza arudi anakubali lakini bado hajarudi nyumbani." Aliongeza.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka sita na wamejaliwa na watoto watatu ambao alienda naye.

Bwana Anthony anakiri kuwa hakuwa na uhusiano na ule mwanadada lakini alichukuana na rafiki ya mkewe.

"Tumeishi naye kwa miaka mitano na huwa tunasumbuana sana na ikafika wakati nikampata na mwanamke fulani na amekuwa na hiyo tabia na ni mjanja pia." Alisimulia Nancy.

Sasa tulipoachana akachukua rafiki yangu wa dhati na akasema huyo ni mwanamke aliyekuwa anamfulia nguo na anampikia. Kwa hivyo amekuwa akinyemelea kabla ya kuiweka wazi." Aliongeza akisema kuwa mbele ya mzee wa mtaa Anthony alisema Eva ndiye mke wake wala sio Nancy.

Anthony alisema kuwa alitaja hayo kwa hasira na kuchanganikiwa na bado anampenda mkewe.

Kama uko side ya Nancy nikate simu? Kwa sababu hakuna vyenye unanisaidia na nilipiga simu ili unisaidie. So am I stranded?" Anthony mwenye hasira alimlipukia Gidi.