PATANISHO: Hata kama atakuwa na mpango wa kando, bado nataka tupatanishwe Mildred asema

patanisho
patanisho
Katika kipindi cha Patanisho leo asubuhi Disemba 6, Bi Mildred alipiga simu studio akiomba anapatanishwe na bwanake ambaye alimtoroka na kumwacha na watoto wao watatu.

Bi Mildred alieleza alivyo na huzuni, maana inaelekea miezi tano tangu bwana Austin ahame.

"Ata silelewi nini nilifanya ju tulikuwa tukikoseana kidog kidogo, hadi siku moja akabebe vitu zetu zote na pikipiki na akaenda zake. Sijui kulikuwaje, akaniacha na watoto. Sasa niko na huzuni, sina kazi natafuta kibarua na watoto watatu wetu'.

Gidi alitaka kujua chenye kilifanya wakosane. Mildred alimjibu akisema, ' Mambo tuu ya wanawake. Alikuwa ananipiga mara kwa mara. Alikuwa ana mpango wa kando na  alitaka niende nyumbani abaki huku nairobi.'

Gidi, 'Mumeooana kwa miaka mingapi na unamiaka mingapi?

Mildred; Tumeoana miaka saba , niko na miaka 24. Nilimuoa nikiwa 16 years. Alinidanganya mimi sikuwa na wazazi na akadanganya nikakubali mambo yake.'

Gidi; Mildred, umesema eti mulikuwa mnaishi pamoja na mpango wa kando?

Mildred; eeh. Nilivumilia kwasababu sikuwa nataka kuenda mahali pengine.

 'Aki huyo mwanume nampenda, juu nikikaa pahali pengine siwezi fikiria mwamume mwingine. Sikudanganyi. Ata akanipiga karibu aniuwe, bado namfikiria; hata kama atakuwa na mwanamke mwingine bado namtaka.'

Gidi akampigia mumewe Austin simu naye akasimulia kulivyo enda.

Austin alieleza kuwa hakuwa amefurahia na tabia za mkewe walipokuwa wakiishi pamoja, ikabidi amwache. Alisema mkewe Mildred alikuwa anachelewa kufika nyumbani, na pia hakuwa anapokea simu zake, pia Mildred aliweza kumaibisha mbele ya wenzake. Kwa hivyo akaamua kumwacha juu ya hizo tabia mbaya.

Mildred aliomba msaaha kwa bwanake, akimwelezea kwa nini anataka amsamehe.

Austin alisema amemsameha, na hawawezi kurudiana kwasababu amesha oa, na kama ni watoto atawashugulikia.

Austin; 'Mimi sina shida nao. Watoto ni wangu na nitawashugulikia. Mimi mambo yangu na yako nisha sahau. Mambo mengine wachana nayo, na tena usinipigie simu ama kutuma message.'

Austin alikata simu na Mildred anashauri hata kama Austin ameolewa, bado bwanake atampata huko nyumbani.

Skiza kanda ifuatayo;