PATANISHO: Huenda familia ya mke wangu wanamshawishi tusikae pamoja asema Baba Blessing

gidinagghostapril20th
gidinagghostapril20th
Wilfred au  Baba Blessing, aliandika amekosana na mke wake na sasa hawaeleweni na ni kama naanaka 50/50, labda kuna watu wengine wanamshawishi wasikae pamoja.

Wapendwa hao wawili walikosana na Wilfred anahofia bibi yake labda kuna mashauri mengine anasikiliza na hataki kurudiana naye.

Walikosana lini na nini kilichotokea?

'ni maneneo ya nyumbani ilitokea, yeneywe ni nmimi nilimkosea nikampiga, sas ameenda miak mbili na miezi nne saa hizi kwasababu nikutoka 2015. Ni mda mrefu na hata kuna kipindi kingine kitambo kidogo ali alikuwa ameenda mwaka na miezi minanae tukiwa na watoto tukiwa na mtoto wetu wa kwanza lakini saa hiyo hakukuwa na vita ama nini na alikuja kurudi. sasa saa hii kulitokea tuu maneno nikampiga.

'mimi ni dereva wa lorry sasa nikienda nikichelewa kazini sababu kama usiku tumeongea nimekuja nyumbani saa saba na saa hizi nimelala kidogo naenda kutoka saa tano nitatoka nianze safari yangu naweza rudi tena late. sasa nikichelewa hivi maneno inatokea ati ohh umeenda kwa wanawake oh ulikuwa wapi, maneno kam hayo yanaleta magombano, sasa ukijaribu kumwongelesha kidogo mnaletana maneni juu ndio hasara ikapandana nikampiga na kutoka saa hiy nilipata ametoroka. 

Wilfred akona miaka 38, na bibi akona miaka 31 na wamekaa kwa ndoa miaka 14.

'Hii December iliyopita nilienda mahali huko anafanyia kazi nikaongea na yeye, tukaongea na tukakubaliana maneneo ya christmas, anakuja nyumbani lakini venye alikuja alienda kwao na nikawatafuta wamam wawili waongee na wazazi wake, na wakarudi na ripoti kwamba wazazi wake wanataka mbuzi mbili.nilizinunua na tukaelekea kwao. kufika huko, bibi yangu akaniambia hana haja na mimi ndio nikatoka nikarudi na mbuzi zangu.

sikuchoka, ilibidi nirudi na nikaongea na yeye akaniambia tena unajua nikuelezee kwa ukweli nikaona huyu mama nikama hatawahi rudi nikaamua kuoa tena, wakati nilioa, baada ya miezi sita, yule mama akaanza kutesa watoto niowacha sababu niliwachwa na watoto wawili na yeye akona kamoja. aliwatesa, akawadhuluma nikaona sitavumulia, nikamwambia wacha nikae peke yangu na watot wangu niwalee mam yao atawhi rudi akijisikia.

sasa ananiambia hawezi ingia nyumba yenye imejengewa mwanamke mwingine, ati nimjengee saa namwabia akuje tuongee tujipange, alee watoto kwasababu wanateseka, wanalalnjaa, 

Skiza kanda