PATANISHO: Jamaa aliniambia yeye ndiye hunichungia mke wangu kazini

patanisho new
patanisho new
Francis Mwangi, kutoka mtaa wa Huruma humu Nairobi alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Elizabeth Nthenya.

Anasema wawili hao ambao wamekuwa kwa ndoa ya miaka 14 walikosana Januari na mkewe kuondoka akimuachia watoto 3.

"Tulikuwa na biashara pamoja na tukaelewana anasafiri siku kadhaa nami nabaki na watoto nyumbani. Sikuelewa mbona hakuwa anataka niende na sikuelewa na nikamuuliza." Alisema Francis.

Sikua najua biashara ilipokuwa na kuna wakati alienda kwa miezi sita na nikaamua kumtafuta. Baadaye tukanunua biashara nyingine ili aweze kurudi nyumbani kwa watoto."

Francis anasema kuwa aligundua baadaye kuwa mkewe alifuta kazi kijana aliyemuandika na kuleta mzee mwingine ambaye ni askari.

Anasema yule jamaa amewahi mpigia mkewe usiku wa manane na alipomuuliza aliambiwa "Mimi ndio huchunga mke wako akiwa kazini"

Isitoshe jamaa anasema wakati alipoenda kumtembelea mkewe alipata ameanza kujipanga na tayari alikuwa amenunua, kiti na meko na vyombo vya nyumbani.

"Wakati nilienda huko huyo jamaa alinipiga pamoja na jamaa mwingine na ni ukweli wana uhusiano na yule askari." Francis aliongeza akisema kuwa mkewe aliondoka hadi na fedha alizoweka akiba.