patanisho

PATANISHO: “Japeth Ni Kama Ana Allergy Ya Wanawake!” – Anita

Hapo jana wanajambo walikuwa mashahidi wa uhondo kamili wakti wa patanisho.

Jamaa kwa jina Japeth aliomba apatanishwe na mkewe Anita ambaye alitoroka nyumbani na mwanao baada ya tabia yake ya kubugia mvinyo kumkasirisha mkewe na kurudi nyumbani baada ya kurudi nyumbani akiwa amelewa chakari

Lakini baada ya mkewe Japeth kupewa nafasi ya kusimulia upande wake , bi Anita aliwashangaza huku akiwachekesha wanajambo baada ya kufichua mengi kumhusu bwanake ambayo hakuwa amesema.

“Ajiheshimu kwanza.” Alifoka Anita.

“Shida sio kulewa kwani nilimpenda vile lakini anapenda wanawake nikama ana allergy ya wanawake. Starehe ndizo anazo chungu nzima ni kama bado hajaamua kufunga ndoa.” Alifichua Anita akisema kuwa mumewe ana tabia mbaya za kuleta wanawake kwake kiholela ili kumuudhi huku akimurai abadilishe mienendo.

“Sijakataa kurudi lakini wacha kwanza nirudi nyumbani nifikirie.” aliongeza anita.

Pata uhondo kamili.

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments