PATANISHO: Jirani yangu aliniseti kwa bibi nina mpango wa kando

Douglass alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Irene.

"Sasa Ghost nilikuwa naishi Kisii na bibi yangu, sasa kuna dem mwingine nilikuwa naye wa kando ambaye alikuja kuniona kwa jirani yangu. Tukaingia kwa nyumba na huyu mwenye nyumba ambaye ni rafiki yangu akapigia bibi yangu simu na kumwambia nina msichana kwa nyumba." Alifichua Douglass.

Mke wangu akatufumania tukiwa tunatoka na tangia siku hiyo mke wangu hajawahi niongelesha, tangia mwezi wa saba mwaka huu. Nikimpigia simu anakataa kuniongelesha akidai hanitaki kamwe." Aliongeza akisema kuwa aliyemuuza ni mzee wa miaka hamsini.

Mkewe alienda kwao na kubeba mwanao.

Aliniletea msichana hadi kwa jirani yangu alipo omba room. Mimi nilikuwa nampigia simu nikiwa nimesimama nje na nikaona pikipiki ikipita na nikamuona na msichana mwingine.

Sasa nilienda huko na nikaingia walimokuwa. Douglass alinitusi na nikamuacha na nikamwambia 'I just came to witness.' Alisema bi Irene akisisitiza aliondoka bila hata kumtusi mumewe.

Mimi naweza tu kusamehe mwendelee na huyo msichana wala sio eti turudiane, madharau ulinionesha mimi sijawahi ona hii dunia tafuta tu mwingine lakini sio mimi. Alisema Irene.

&feature=youtu.be