PATANISHO: Kama Hataki Kusomesha Mtoto Wake, Wangu Ndio Ataweza?

Bonny alituma ujumbe akisema kuwa angependa apatanishwe na mkewe Josphine ambaye walikosana na kutengana wiki tatu zilizopita.

"Saa hizi tunapozungumza yuko kwao nyumbani. Nilielekea kazini kule Namanga na niliporejea nyumbani sikumpata. Kumpigia simu akanieleza yuko nyumbani na kuuliza mbona akaamua vile akasema kuwa nilimkosea, ila sikufanya lolote." Alieleza baba Brighton.

Isitoshe kuna siku nikiwa kazini Namanga na hapo nilipigiwa simu kuwa mke wangu alikuwa ametupa mtoto wangu kwa ploti, isitoshe nilielezwa kuwa mtoto alitupwa kwa mlango na alikuwa tayari ameondoka. Kuulizwa akadai kuwa pia mtoto ana babake na pia yeye anaweza mlea." Aliongeza Bonny mwenye umri wa miaka 30.

Mkewe ana miaka 25, na wawili hao wana watoto wawili.

Alipopigiwa simu mamake Josphine alisisitiza kuwa kama mwanawe anataka kuomba msamaha, afunge safari aelekee nyumbani akaombe msamaha.

"Wewe una makosa na lazima uje nyumbani uombe msamaha. Lazima usafiri kwani kuna mambo mengi tunafaa kusuluhisha." Alisema huku akisema kuwa hamna yeyote aliye na mipango ya kumpa kichapo.

Josephine alipopata fursa ya kuzungumza alisema kuwa mumewe shida ni ya ujinga nyingi na hamskizi. "Nikimueleza aje tujenge nyumbani hataki kuskia anataka tu kuishi Nairobi. Kisha anamtusi mamangu na hataki kusaidia mtoto wangu ambaye alinioa naye na nikimsaidia hataki hayo maneno."

Pata uhondo wote.

&feature=youtu.be