PATANISHO: Kama tunarudiana mimi ndio first lady! - Anita

patanishoo (1)
patanishoo (1)
Anita, 26, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na baba mtoto bwana Robert akidai kuwa wawili hao walikosana mwaka wa 2016.
"Alikuwa boy wangu na wakati nilimuambia nina mimba yake ndipo alipoanza kubadilika na kwenda kwake nikapata tayari ana bibi, licha ya kuahidiana kuwa tutaoana." Alisema Anita.

Aliongeza,

Imagine Gidi nilimkubali jinsi alivyo hadi nikaharibu kazi yangu kwa kuwa nilikuwa nampenda na akanifanyia hivi. Yule mke wake tulizungumza na nikama alitaka tupigana sasa nikatoka kwa sababu Robert hakuwa."

Anasema kuwa Roba tangia amkane hajawahi hata mpigia simu kujua jinsi mtoto alivyo. Isitoshe anakiri wazazi wake walimfukuza kwao kwa kupata mimba na yuko tayari kurudiana na Roba hata kama ni kuwa mke wa pili.

Kuna boy tulikuwa tuna push na yeye na akaniambia hawezi oa mtu ana mtoto.

"Wewe si ulianza matusi kuwa mimi ni maskini eti siwezi kusaidia, ulianza hayo matusi hata kabla nioe. Ulimaliza morale kwani ukiniita maskini na kuna mwenye amekubali umaskini wangu nitafanyaje?" Alijitetea Roba.

Aliuliza,

Mimi ni hustler, mke wa pili nitatoboa aje?

Robert anasema kuwa atajipanga ajue jinsi atamchukua Anita kama mke wa pili lakini Anita anasema ako tayari kurudiana lakini atatambulika kama mke wa kwanza.