PATANISHO: Mimi nataka Lucy, huyo mwanamke mwingine ni expensive!

Bwana Achimba alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Lucy ambaye walikosana mwaka wa 2016.

"Huwa tunazungumza naye lakini hatujazungumza kuhusu mambo ya kurudiana ila ni mambo ya watoto.

Tulikosana baada yake kuanza madharau na nikakasirika nikavunja simu yake. Isitoshe nilikuwa na tabia za kunywa pombe na kuwa na mipango za kando." Alieleza Achimba.

Alipopigiwa simu bi Lucy alidai anamfahamu Achimba kama baba wa watoto wao.

"Sasa tuaongalie watoto aje na ulibeba mtoto mmoja? Kama unataka tuzungumze chochote unirudishie mtoto." Aliuliza Lucy akidai kuwa bwanake ana bibi na hana kwa kurudi.

Imagine alikuja akachukua mtoto nyumbani akiwa mchafu nyumbani na nimejaribu kumwambia amrudishe nashindwa. Isitoshe ana bibi na am very sure." Aliongeza.

Bwana Achimba alifichua kuwa baada ya kuwachana na Lucy alitafuta mke mwingine ambaye alikuwa anaishi kwake, lakini mtoto wake hakuwa anampenda na pia mamake Achimba hakumkubali.

"Huyo mwanamke ni expensive sana, unajua Lucy ukimuachia elfu moja unajua utakula lakini yule mwingine ukimuachia fedha bado ataitisha za maziwa." Alisema.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be