PATANISHO: Mimi staki maneno ya Patanisho kabisa sina huo mda! - Teresa

Festus aliomba apatanishwe na mkewe bi Teresa, waliyewachana miaka minne iliyopita kwa sababu ya fitina za watu.

Anasema wamejaliwa watoto wawili.

Tulipatana mtoto kabla hatujaoana na wakati tulioana tukajaliwa mtoto mwingine na tulikuwa tunaishi vyema. Sasa msichana ambaye tulikuwa na uhusiano kitambo akaanza kunitumia ujumbe na mke wangu akashuku kuna mambo.

Festus alisema kuwa Teresa alijaribu kujitia kitanzi ila aliokolewa. Hapo alirudi shule na akaanza kumtumia ujumbe mbaya na baadaye yule mkewe akadai hataki maneno yake.

Mkewe aliondoka na watoto na kwenda nao kwao.

Festus aliongeza,

Tulikuwa tunazungumza na wazazi wa bibi ila hawataki turudiane. Nilikuwa na mpenzi mwingine ila hakutaka kusaidia watoto wetu sasa nikaamua heri tu nirudiane na yule mke wangu." 

"Mimi staki maneno ya Patanisho kabisa sina huo mda kwani kila kitu mnataka kuniambia najua." Teresa alisema baada ya kupigiwa simu kabla ya kukata simu.

Isitoshe alisema hakutakuwa na msamaha baina yao wawili na patanisho ya leo ikashindikana.

Je ni mawaidha gani waweza mpa bwana Festus ambaye anakiri anasononeka moyoni?